kwenye kamusi

Misukosuko ya hatua za ukuaji (developmental crises)

Misukosuko ya hatua za ukuaji ni vipindi vya mabadiliko katika maisha ya mtu anapohama kutoka hatua moja ya ukuaji wake kwenda nyingine. Katika kila mabadiliko hayo, mtu hukabili majukumu mapya yanayohusiana na umri huo.

Katika tafiti zake, L. S. Vygotsky alianzisha dhana ya “msukosuko wa hatua ya ukuaji” katika saikolojia ya Umoja wa Kisovieti. Alieleza misukosuko hiyo kuwa mabadiliko makubwa katika haiba ya mtoto wakati wa mpito kati ya hatua thabiti za ukuaji. Tafiti zinaonyesha kwamba misukosuko ya hatua za ukuaji inaweza kuathiri sana maisha ya mtu. Kwa mfano, vijana walio katika kipindi cha mpito cha kubalehe mara nyingi huonyesha tabia hasi, kama vile uasi na migogoro na watu wanaowazunguka.

Hata hivyo, si watafiti wote wanaoona tabia hii kuwa sehemu isiyoepukika ya msukosuko huo. Baadhi wanaona kwamba tabia hasi katika kipindi hiki inaweza kutokana na uhusiano usiofaa kati ya mtoto na watu wazima.

Kwa vyovyote vile, misukosuko ya hatua za ukuaji ni vipindi vya changamoto na mabadiliko katika maisha ya mtu vinavyoweza kuathiri ukuaji wake na namna anavyojielewa.