kwenye kamusi

Ugonjwa wa bipola (bipolar)

Ugonjwa wa bipola (bipolar) ni hali ya kiafya inayojitokeza kwa kupishana kwa vipindi vya kupanda na kushuka kwa hali ya hisia, nguvu na kiwango cha shughuli. Vipindi hivi hujulikana kama vipindi vya hali ya hisia iliyopanda kupita kiasi (mania), au iliyopanda kwa kiwango kidogo zaidi (hypomania), na vipindi vya sonona (depression).

Katika vipindi vya hali ya hisia iliyopanda kupita kiasi, mtu anaweza kuhisi furaha kubwa sana, kuwa na nguvu nyingi kupita kiasi, kufikiri kwa kasi zaidi na kufanya vitendo hatarishi bila kutathmini matokeo yake. Kwa upande mwingine, vipindi vya sonona huwa na hali ya hisia iliyoshuka, kupoteza hamu au kutopata furaha katika shughuli nyingi, pamoja na mawazo ya kujidhuru au kujiua.

Ili kudhibiti hali hii, zinahitajika mbinu zinazoshughulikia vipengele mbalimbali, zikiwemo matibabu kwa dawa, msaada wa kisaikolojia na marekebisho ya mtindo wa maisha. Kila hali ya ugonjwa wa bipola ni ya kipekee, hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa kina na kuandaa mipango ya matibabu inayolingana na mahitaji ya kila mtu.