kwenye kamusi

Hali ya kupoteza uhalisia (psychosis)

Hali ya kupoteza uhalisia (psychosis) ni ugonjwa wa akili wenye uzito mkubwa unaoathiri uwezo wa kutofautisha uhalisia na mambo ya kufikirika na kusababisha mawazo na tabia kukosa mpangilio unaoeleweka. Hali hizi zinaweza kujitokeza kwa njia mbalimbali na kuwa na visababishi na dalili tofauti. Zifuatazo ni baadhi ya sifa zake kuu:

  1. Kupoteza uhusiano na uhalisia: Watu wenye hali hii wanaweza kuhisi vitu ambavyo havipo (hallucinations), kutambua vitu vilivyopo kwa namna iliyopotoka (illusions) na kuwa na imani potofu (delusions) ambazo hazibadiliki hata wengine wanapojaribu kuwashawishi kuziacha.

  2. Kuvurugika kwa kufikiri: Hali hizi mara nyingi huambatana na kuvurugika kwa mantiki ya mawazo. Watu wanaweza kuzungumza bila mpangilio unaoeleweka, kuruka kutoka wazo moja hadi jingine au kueleza mawazo yanayotokana na imani potofu zisizobadilika.

  3. Mabadiliko ya hisia: Hali hizi zinaweza kusababisha hisia kali, kama vile hofu, wasiwasi, furaha iliyopitiliza au kutojali.

  4. Uwezo wa kushiriki katika maisha ya kijamii na kufanya kazi: Hali hizi mara nyingi huambatana na matatizo makubwa ya tabia na mahusiano ya kijamii. Watu wanaweza kupoteza uwezo wa kujitunza, kuwasiliana na wengine na kutekeleza majukumu ya kawaida.

  5. Visababishi: Hali hizi zinaweza kuwa na visababishi mbalimbali, vikiwemo sababu za kijenetiki, msongo wa mawazo, dawa za kulevya na pombe, maambukizi, majeraha na sababu nyingine.