kwenye kamusi

Kutoweza kutambua vitu kwa kuona (visual agnosia)

Kutoweza kutambua vitu kwa kuona (visual agnosia) ni tatizo la utambuzi ambapo mtu hawezi kutambua vitu kwa kuviona, licha ya kutokuwa na matatizo ya kuona. Hali hii inaweza kutokea kutokana na uharibifu wa ubongo na kwa kawaida huhusishwa na sehemu ya nyuma ya ubongo upande wa kushoto au sehemu za pembeni za ubongo zilizo karibu na masikio. Hali hii imegawanyika katika aina mbili: kushindwa kuunda taswira kamili ya kitu kinachoonekana (apperceptive agnosia), ambapo mtu hawezi kunakili maumbo kwa kuchora au kulinganisha maumbo; na kushindwa kuhusisha taswira na maarifa kuhusu kitu (associative agnosia), ambapo taswira huundwa lakini haihusishwi na maarifa kuhusu kitu hicho: mtu anaweza kunakili kitu kwa kuchora lakini hakitambui.